Msururu wa magari ya kubeba mafuta hadi kilometa 70 unaripotiwa kwenye mipaka hiyo.
Madereva wa magari ya kusafirisha mafuta wamekuwa wakilalamikia hatua ya serikali ya Uganda kwamba ni lazima wafanyiwe vipimo vya corona hata kama wana vyeti vinaonyesha kwamba hawajaambukizwa virusi hivyo.
Amri hiyo ambayo ilitolewa mwezi uliopita, iliondolewa baadaye lakini tayari msongamano wa magari hayo mipakani ulikuwa tayari mkubwa.
Uganda huagiza mafuta ya petrol na bidhaa nyinginezo.
Karibu lita milioni 6.5 za petrol hutumika Uganda kila siku.
Bei ya mafuta imekuwa ikiongezeka tangu mwaka uliopita, na kufikia kiwango cha juu zaidi wiki iliyopita.
Lita ya petrol inauzwa shilingi 5,200, saw ana dola 1.5, jijini Kampala.
Wizara ya nshati imetoa amri kwa vituo vyote vya kuuza mafuta kuuza lita ya mafuta kwa bei ya shilingi 5000.
Katika sehemu nyingine za nchi, lita moja ya Petrol inauzwa shilingi 10,000 na baadhi ya sehemu zinaripoti uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo.