Serikali ya Israel siku ya Jumatano imesema itachangia chanjo milioni 1 za virusi vya corona kwa mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa COVAX.
Wizara ya Mambo ya Nje ilisema chanjo za AstraZeneca zitahamishwa katika wiki zijazo, uamuzi ambao ulikuwa sehemu ya kuimarisha uhusiano wa Israeli na nchi za Kiafrika.
Nimefurahi kuwa Israeli inaweza kuchangia na kuwa mshirika katika kutokomeza janga hili ulimwenguni, Waziri wa Mambo ya nje Yair Lapid alisema.
Tangazo hilo lilisema kuwa chanjo hizo zitafikia karibu robo ya nchi za Afrika, ingawa haikutoa orodha. Israel ina uhusiano wa karibu na mataifa kadhaa ya Afrika, yakiwemo Kenya, Uganda na Rwanda. Israel pia ilianzisha uhusiano na Sudan mwaka jana kama sehemu ya mfululizo wa mapatano yaliyosimamiwa na Marekani.