Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 11:18

Washukiwa wa ugaidi 15 wafikishwa mahakamani Uganda


Kiongozi wa kundi la waasi wa ADF Jamil Mukulu akifikishwa katika mahakama kuu ya Uganda jijini Kampala, May 14, 2018.
Kiongozi wa kundi la waasi wa ADF Jamil Mukulu akifikishwa katika mahakama kuu ya Uganda jijini Kampala, May 14, 2018.

Watu 15 wamefikishwa mahakamani nchini Uganda na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi kuhusiana na mashambulizi ya mabomu yaliyotokea katika jiji kuu la Kampala na sehemu zingine za nchi kati ya mwezi Oktoba na Novemba mwaka huu.

Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya watu tisa. Washukiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutengeneza mabomu na kupanga namna yatakavyolipuliwa, wakiwa na lengo la kuua au kujeruhi, Pamoja kusababisha hofu nchini Uganda.

Mlipuaji wa kujitoa mhanga alijilipua nje ya kituo kikuu cha polisi katikati mwa Kampala, kabla ya bomu mengine mawili kulipuka karibu na majengo ya bunge, Novemba tarehe 16.

Watu saba waliuawa katika shambulizi hilo wakiwemo walipuaji. Watu wengine kadhaa walijeruhiwa. Shambulizi lingine lilitokea mwezi Oktoba katika mgahawa na kuuwa mtu mmoja huku shambulizi lingine ndani y abasi likiua mtu mwingine.

Kundi la kigaidi la Islamic state, lenye ushirikiano na kundi la waasi wa Allied democratic forces ADF linalojifisha mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya congo, limedai kuhusika na mashambulizi hayo. Washukiwa watasalia rumande hadi Januari 13, watakaporejeshwa mahakamani kwa mara nyingine.

XS
SM
MD
LG