Foleni ndefu ya magari ya kubeba mizigo inashuhudiwa kwenye barabara kuu ya kutoka Eldoret hadi Malaba Kenya, kutokana na mwendo wa pole wa kuruhusu magari hayo kupita mpakani kufuatia vipimo vya Corona kwa madereva.
Madereva wamelalamika kwamba hatua ya kufanyiwa vipimo mara mbili mpakani haifai kabisa na kwamba inasababisha foleni ya magari.
Dereva mmoja amesema kwamba alipewa cheti cha kuonyesha kwamba hajaambukizwa Corona akiwa Kenya, lakini alilazimishwa kufanyiwa vipimo kwa mara nyingine alipoingia Uganda.
Foleni ndefu ya magari iliyoanza wiki kadhaa zilizopita, imefika umbali wa kilomita 140.
Mnamo mwezi May 2020, madereva wa magari ya kubeba mizigo walilalamika kuhusu vipimo vya corona mpakani, na kupelekea kufungwa kwa barabara kuu kati ya Kenya na Uganda kwa muda wa wiki tatu.