Somaliland ilijitenga na somalia zaidi ya miaka 30 iliyopita lakini haitambuliwi kama taifa huru na umoja wa Africa au umoja wa mataifa.
Wizara ya mambo ya nje ya Somaliland imekaribisha hoja hiyo na kutoa wito kwa wakazi wake nchini Uingereza kuwasiliana na wabunge wao kuhusu suala hilo.
Serikali za mitaa za Uingereza katika miji ya Sheffield, Cardiff na Birmingham zinaunga mkono uhuru wa Somaliland, lakini serikali ya Uingereza haiungi mkono.