Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 12:28

Watu wawili wakamatwa DRC kuhusiana na mauaji ya balozi wa Italia


Hayati Luca Attanasio
Hayati Luca Attanasio

Maafisa mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamewakamata wanaume wawili kuhusiana na kuuawa kwa balozi wa Italia mwaka 2021, japo polisi wamesema kwamba washukiwa wakuu wa mauaji hayo bado wanatafutwa.

Jenerali Aba van Ang, Mkuu wa Polisi katika jimbo la Kivu Kaskazini, amesema kwamba waasi walimuua balozi Luca Attanasio katika jaribio la kumteka nyara ili walipwe fidia.

Washukiwa ambao wamefikishwa kwa Gavana wa Kijeshi katika jimbo hilo, na kuonyeshwa mbele ya waandishi wa habari, wamesema kwamba walikuwa wamepanga kudai kiasi cha dola milioni 1 endapo wangefanikiwa kumteka nyara balozi huyo.

Badala yake, balozi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 43 alipigwa risasi na kuuawa, Pamoja na afisa wa kijeshi Vittorio Iacovacci na dereva wa shirika la chakula la umoja wa mataifa Moustapha Milambo.

Jeneral Constant Ndima Kongba, Gavana wa Kijeshi wa Jimbo la Kivu Kaskazini anaeleza: "Tutaendelea kufanya kazi. Mmefanya kazi ya kubwa. Tutaendelea kuharibu hii mitandao yote ya uhalifu popote ilipo. Tutashirikiana na idara nyingine za usalama katika sehemu zote huko Kkvu Kusini, Maniema, Ituri, na hata marafiki zetu katika nchi jirani kama Uganda na Rwanda ili kuyasambaratisha haya makundi ya uhalifu.

Hawa wahalifu wanayweka majimbo katika maombolezo. Ni lazima tuhakikishe kwamba watu wetu wana amani."

XS
SM
MD
LG