Hayo ameyasema baada ya kula kiapo cha kuanza muhula wake wa pili madarakani. Barrow mwenye umri wa miaka 56, aliingia madarakani mwaka 2017 baada ya kumshinda kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo Yahya Jammeh.
Barrow kwenye uchaguzi wa mwezi uliopita lisinda kwa asilimia 53 ya kura zilizopigwa . Katika muhula wake wa kwanza, aliboresha mahusiano na mataifa mengi ya nje ambayo hayakuwa katika nafasi njema mzur wakati wa utawala wa Jammeh wa miaka 22. Barrow amejitahidi kurejesha uhuru wa watu ambao ulikuwa umekandamizwa katika kipindi chote cha nyuma wakatiw a utawala wa Jammeh
Alipoingia madarakani,alikabiliwa na changamoto ya kufufua uchumi wa taifa hilo dogo zaidi la barani Afrika. Janga la virusi vya corona liliusukuma uchumi kuingia katika msukosuko mwaka 2020 na kuwafanya watalii kutotembelea fukwe nzuri za taifa hilo.