Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 20:44

Mwandishi wa vitabu na mkosoaji wa rais wa Uganda, aachiliwa kwa dhamana


Rais wa Uganda Yoweri Museveni akisalimia umati wa watu kabla ya sherehe za kuapishwa kwa muhula wa sita, Mei 12, 2021. Picha ya AP
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akisalimia umati wa watu kabla ya sherehe za kuapishwa kwa muhula wa sita, Mei 12, 2021. Picha ya AP

Mwandishi wa vitabu nchini Uganda Kakwenza Rukirabashaija ameachiliwa kwa dhamana leo Jumanne, wakili wake amesema lakini inaripotiwa kwamba alichukuliwa mara baada ya kuachiwa na hajulikani alipo.

Rukirabashaija, mkosoaji mkubwa wa rais Yoweri Museveni alikamatwa mwezi Disemba na kushikiliwa na vyombo vya usalama bila kuelezewa mashtaka yanayomkabili na bila kuruhusiwa kuzungumza na mtu yeyote wa nje hadi Januari 11, ambapo alishtakiwa kwa makosa ya mawasiliano ya kukashifu.

Rukirabashaija amekuwa akiwakosoa kwenye mitandao ya kijamii rais Museveni na mtoto wake Muhoozi Kainerugaba.

Kwenye mtandao wa Twitter aliandika rais ni mwizi wa kura na kwamba mtoto wake hana akili timamu.

Katika kikao cha kuachiwa kwa dhamana, Rukirabashaija aliamriwa kulipa shilingi 500,000, kupana pasipoti yake na kutozungumzia suala hilo kwenye vyombo vya habari.

Awali, wakili wake Eron Kiiza aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba mteja wake aliteswa akiwa gerezani.

XS
SM
MD
LG