Maelfu ya mashabiki walijipanga barabarani kwenye Kilometa za mwisho za mashindano hayo huko Paris, kuelekea kwenye msitari wa kumaliza mbio hizo kwenye majengo ya kijeshi ya Invalides mjini Paris.
Bashir Abdi wa Ubelgiji alitwaa medali ya fedha, ambayo ni bora kuliko shaba aliyoipata mjini Tokyo, Japan, huku Mkenya Benson Kipruto alijinyakulia shaba.
Tola alianza kuongoza mapema na kuvuka mstari wa kumaliza kwa muda wa saa mbili, dakika sita na sekunde 26.
Akiibuka kutoka kundi la wakimbiaji waliokuwa mbele katika mteremko wa kwanza wa aina yake unaopanda mlima, bingwa huyo wa zamani wa mbio za nyika alionekana kujiimarisha punde alipofika kwenye mlima wa pili wakati wengine wakififia nyuma yake.
Amekuwa MuEthiopia wa kwanza kushida mashindano hayo ya Olimpiki ya mbio za marathoni za wanaume katika kipindi cha miaka 24.
Tola alikuwa akiongoza kwa sekunde 18 kwa umbali wa kilometa 35, ambapo aliongeza kasi wakati mnara wa Eiffel ulipoonekana huku umati wa watu waliokuwa wamejipanga barabarani wakimshangilia.
Tola mwenye umri wa miaka 32 alishinda mbio za marathoni za New York mwaka jana na kuvunja rekodi.
Forum