Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:43

Mto Nile : Ethiopia, Misri na Sudan zakaribia kufikia makubaliano ya tofauti zao


Mradi wa Grand Ethiopian Renaissance Dam unaoendelea kujengwa nchini Ethiopia, Sept. 26, 2019.
Mradi wa Grand Ethiopian Renaissance Dam unaoendelea kujengwa nchini Ethiopia, Sept. 26, 2019.

Waziri wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Sudan Yasser Abbas amesema kwamba Misri, Ethiopia na Sudan zinakaribia kutanzua tofauti zao juu ya utumiaji na usimamizi wa bwawa la kuzalisha umeme linalojengwa na Ethiopia.

Tangazo hilo limetolewa baada ya mawaziri wa nchi hizo tatu kukutana mjini Khartoum mwishoni mwa wiki.

Hofu ya Misri

Misri ilikuwa na wasiwasi kwamba mradi wa Grand Ethiopia Renaissance Dam, GERD, unaojengwa wakati huu karibu na mpaka kati ya Ethiopia na Sudan, kwenye mto wa Blue Nile, utapunguza maji ambayo tayari yamepungua sana katika mto Nile inayotegemea sana.

Na kwa muda wa miezi kadhaa hivi karibuni nchi hizi tatu zimekuwa zikikutana kujaribu kufikia makubaliano juu ya matumizi ya bwawa hilo.

Waziri huyo aliwaambia waandishi wa habari Jumapili baada ya kukutana na mawaziri wenzake kutoka Misri na Ethopia kwamba mapendekezo yamewasilishwa na mataifa hayo matatu kuhusu kujaza bwawa na usimamizi wake na hapo mawazo yalikuwa yanakaribiana.

Habari nyeti za kiufundi

Abbas amesema : “Kulikuwepo na habari muhimu na nyeti za kiufundi tulizobadilishana na kupelekea kuongezeka ushirikiano kati ya nchi zetu tatu. Hili ilikuwa ni pamoja na kueleza maana halisi ya ukame na ukame unaodumu. Kulikuwepo na makubaliano juu ya kuchukua misimamo hii mipya. Kila nchi inakamilisha utafiti wake tayari kwa kuwasilisha katika mkutano ujao wa Addis Ababa Januari 2-3, 2020.

Hapo mwezi Novemba mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Ethopia, Misri na Sudan walikubaliana kufanya kazi pamoja kutanzua ugomvi wao juu ya bwawa litakalo gharimu dola bilioni 4 ifikapo Januari 15, 2020, baada ya kukutana na Waziri wa Fedha wa Marekani Steven Mauchin na Rais wa Benki kuu ya Dunia David Malpass mjini Washington.

Mawaziri hao watakutana tena hapa Washington mwisho wa Disemba na mkutano wa tatu utakaofanyika Januari 13, ambapo watakamilisha makubaliano ya kutanzua kabisa mvutano uliopo kati yao.

Serikali ya Marekani yawapatanisha

Serikali ya Marekani ilizialika pande hizo tatu baada ya Misiri kutoa wito wa kuwepo na mpatanishi kutoka nje ikisema mkutano wa pande tatu umeshindwa kuzaa matunda. Ethopia awali ilipinga wazo hilo ikidai Misri inajaribu kukwepa utaratibu waliokuwa nao.

Waziri Abbas alisema Jumapili walikubaliana kurudi na tafsiri ya ukame na jinsi bwawa hilo litakavyofanya kazi wakati wa kipindi cha ukame .

Msimamo wa nchi hizo

“Bila shaka kuna maelewano mazuri kati ya misimamo ya nchi zetu. Kwa ujumla mawazo yanafanana, hata hivyo kuna tofauti katika baadhi ya mambo ambayo kila nchi itatafakari kabla ya mkutano wa Addis Ababa,” amesema

Kwa upande wake Misri imesema walitaka kufikia makubaliano juu ya namna ya kujaza na kuendesha bwawa hilo jambo ambalo limezishawishi nchi zote tatu katika njia ya kuhifadhi mto huo kwa maslahi ya pamoja.

XS
SM
MD
LG