Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:02

Msumbiji: Balozi GreenField aeleza juhudi kubwa yahitajika kuwaondoa waasi Cabo Delgado


Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa Thomas Greenfield Ukraine
Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa Thomas Greenfield Ukraine

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas Greenfield anasema juhudi kubwa zinahitajika nchini Msumbiji kuwasukuma waasi ambao wasambaa kusini kutoka kaskazini katika jimbo la Cabo Delgado.

Greenfield alikuwa nchini Msumbiji Ijumaa katika ziara yake ya mataifa matatu ya Afrika.

Akizungumza katika mkutano wa wana habari katika siku ya mwisho ya ziara yake siku mbili, Greenfield alisema Marekani iko tayari kufanya kazi na Msumbiji katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mapema mwezi huu, Msumbiji ilichukua kiti cha uanachama wa mwaka mmoja ambacho si cha kudumu katika Baraza la Usalama.

Ilikuja wakati ambapo uasi wenye silaha katika jimbo la Cabo Delgado, upande wa kaskazini mwa nchi, bado ni changamoto kuu ya usalama, huku baadhi ya mashambulizi yakidaiwa kufanya na kundi lenye msimamo mkali la Islamic State.

“Tumeongeza maradufujuhudi zetu kusukuma vitendo vya kigaidi. Harakati ambazo zinawatisha raia wa kawaida kama vile raia wa Cabo Delgado, na tunafanya kazi kwa karibu na serikali kushughulikia masuala hayo,” amesema Balozi Greenfield.

Greenfield, ambaye alianza ziara yake ya Afrika nchini Ghana siku ya Jumatano, atakwenda Kenya akitoka Msumbiji.

Kundi la uasi nchini Msumbiji ambalo linajiita Ansar Al Sunna, au Followers of Tradition, lakini linajulikana kote nchini Msumbiji ka al-Shabab. Halina uhusiano ambao unajulkana na kundi lenye jina kama hilo la huko Somalia.

LImekuwa likikalia wilaya kadhaa katika jimbo la Cabo Delgano tangu mwaka 2017.

Mpaka hivi leo kiasi cha watu 5,000 wameuawa katika mashambulizi na takriban milioni 1 wamekoseshwa makazi kwa mujibu wa taasisi za kibinadamu.

XS
SM
MD
LG