Balozi Linda Thomas-Greenfield, Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, atakwenda Ghana, Msumbiji na Kenya Januari 25 hadi 29 kuthibitisha na kuimarisha ushirikiano wa Marekani na wanachama muhimu wa sasa na wa zamani wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kufuatia Mkutano wa Viongozi wa Marekani na Afrika uliofanyika Disemba mwaka jana, ziara ya Balozi Thomas-Greenfield itaendeleza vipaumbele vya pamoja, ikiwa ni pamoja na kushughulikia usalama wa kikanda, kuimarisha ahadi za demokrasia na haki za binadamu, kuimarisha usalama wa chakula, kusaidia ustahimilivu wa Afrika na kupona, na kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Nchini Ghana, Balozi Thomas-Greenfield ataangazia ziara yake ya Agosti 2022, ikiwa ni pamoja na mikutano na viongozi wanawake na asasi za kiraia. Nchini Msumbiji, Balozi Thomas-Greenfield atajadili ushirikiano thabiti baina ya nchi hizo mbili na kuikaribisha Msumbiji katika muhula wa kwanza wa kihistoria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Balozi pia atakutana na maafisa wa Umoja wa Mataifa, wajumbe katika program za tathmini za maendeleo, wanafunzi, na wanachama wa asasi za kiraia, ikiwa ni pamoja na wale wanaohusika katika hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini Msumbiji.
Akiwa nchini Kenya Balozi Thomas-Greenfield atapewa maelezo kutoka kwa timu ya Umoja wa Mataifa nchini humo kuhusu mipango ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na ukame wa kikanda na msaada kwa wakimbizi. Balozi Thomas-Greenfield atakutana na wakimbizi wanaosubiri makazi mapya nchini Marekani na kuelezea mpango mpya ulioanzishwa na Utawala, Welcome Corps. Pia atakutana na wajasiriamali wa Kenya waliopo mstari wa mbele katika kipindi cha mpito cha nchi hiyo kuelekea uchumi wa kijani. Ziara ya Balozi huyo pia itaangazia athari za vita vya Russia dhidi ya Ukraine vinavyoendelea kusababisha ukosefu wa usalama wa chakula duniani, ambao umezidisha mzozo wa kibinadamu katika eneo hilo.