Miongoni mwa washtakiwa 19 walioshtumiwa katika kashfa kubwa nchini humo ni mtoto wa rais wa zamani Armando Guebuza, Ndambi Guebuza, mkuu wa zamani wa idara ya usalama na ujasusi, Gregorio Leao, na mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi kuhusu masuala ya uchumi ambaye aliongoza kampuni tatu za serikali zilizokopa mabilioni ya pesa katika njia isiyo halali, Antonio do Rosario.
Washtakiwa wanane waliachiwa huru huku waliobaki wakipewa kifungo cha kati ya miaka 10 na 12.
Kashfa hiyo iliibuka baada ya kampuni za serikali katika nchi hiyo kukopa kinyume cha sheria dola bilioni 2 mwaka wa 2013 na 2014 kutoka benki za kimataifa ili kununua meli ya uvuvi na meli za usalama.