Bidhaa hizo ni pamoja na sabuni za maji za kuogea, shampoo krimu na zile za kupuliza.
Mamlaka inasema bidhaa hizo vitu ambavyo vinaweza kusababisha saratani, ikiongezea kuwa ni hatari kwa afya ya uzazi na pia vinaweza kusababisha kutokuwa na uwezo wa kushika mimba
EU ilionya dhidi ya matumizi ya bidhaa hizo mapema mwezi Septemba, alisema Sheila Mercis mkaguzi katika mamlaka ya kufuatialia dawa nchini humo ANARME.
Watengenezaji wa bidhaa hizo tayari wamewasilisha aina mpya ya vipodozi ambavyo ANARME ilivitaja ili kupata idhini kusudi viwezei kuagizwa tena kutoka nje lakini vikiwa ‘havina vitu ambavyo ni hatari’ kwa binadamu.