Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:00

Mlipuko kambi ya jeshi Goma waua 6 na kujeruhi 15


FILE - Wanajeshi walinda amani wakiwa katika kituo kipya cha kijeshi huko Rugari, kilomita 50 kutoka mji wa Goma mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jan. 28, 2022.(Photo by Glody MURHABAZI / AFP)
FILE - Wanajeshi walinda amani wakiwa katika kituo kipya cha kijeshi huko Rugari, kilomita 50 kutoka mji wa Goma mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jan. 28, 2022.(Photo by Glody MURHABAZI / AFP)

Takriban watu sita wameuwawa na wengine 15 wamejeruhiwa baada ya mlipuko kutokea katika baa kwenye kambi ya kijeshi ya Katindo mjini Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Wizara ya Mawasiliano iliandika katika ukurasa wake wa Twitter jana usiku kuwa idadi ya walioathiriwa ni ya awali, huku ikirekebisha idadi kubwa ya vifo iliyotangazwa na msemaji wa serikali Patrick Muyaya.

Miongoni mwa waliojeruhiwa ni pamoja na Luteni Kanali na mkewe, Kapteni, mmiliki wa baa hiyo na rafiki yake pamoja na kijana wa miaka 12.

Mamlaka za ndani zinafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo. Mwishoni mwa mwaka 2020, serikali ilitangaza kwamba kambi ya kijeshi ya Katindo itahamishiwa nje ya mji ili kupunguza ukaribu wake na wakazi wa Goma, ambao ni takriban milioni mbili.

Hili hata hivyo halijatekelezwa. Jeshi la DRC linapambana na makundi mawili ya waasi mashariki mwa nchi, lakini halina uhakika kama mlipuko ulikuwa ni matokeo ya shambulizi.

Gavana wa Kivu kaskazini ametoa wito kwa watu kuwa na utulivu na kuepuka uzushi wakati uchunguzi unaendelea.

XS
SM
MD
LG