Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:34

Mapigano makali kati ya M23 na FARDC yanaendelea DRC


Wanajeshi wa DRC wakishika doria karibu na Rutshuru katika mapambano na waasi wa M23. PICHA: AFP
Wanajeshi wa DRC wakishika doria karibu na Rutshuru katika mapambano na waasi wa M23. PICHA: AFP

Mapigano makali yanaendelea kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, yanaendelea mashariki wa DR Congo karibu na mpaka na Uganda, katika sehemu za Runyoni, Kinyamahura, Kanombe na Jomba, Mkoa wa North Kivu.

Mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa DRC yanajiri wakati kuna mipango ya kufanyika kikao cha usalama Jijii Nairobi Kenya, kusikiliza mambo yanayowakera waasi wa m23.

Kundi la M23 lilikuwa limetangaza kusitisha mapigano wiki iliyopita, baada ya makabiliano mabaya mashariki mwa DRC ambapo watu kadhaa na wanajeshi kuuawa. Maelfu ya watu walikimbilia Uganda.

Msemaji wa kundi la M23 Mj. Willy Ngoma, ameukuliwa na vyombo vya habari vya DRC akisema kwamba kundi hilo limekataa kusitisha vita na kufanya mazungumzo na serikali ya DRC.

Mkutano kato ya rais wa Uganda Yoweri Museveni, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Felix Tshisekedi wa DRC unatarajiwa kufanyika kutafuta suluhisho la mapigano hayo.

Haijabaibika iwapo ni wanajeshi wa DRC waliotanguliwa kushambulia waasi hao katika mapigano mapya ama ni waasi ndio walianza kushambulia wanajeshi wa serikali.

Uganda yaimasrisha usalama mpakani

Katika kikao na waandishi wa habari mapema wiki hii, msemaji wa polisi wa Uganda Fred Enanga, alisema kwamba wanajeshi wa DRC walikuwa wanapanga kushambulia sehemu walipo wapiganaji wa M23, kusini mashariki mwa DRC na kwamba wanajeshi wa Uganda wameimarisha usalama mpakani kuzuia mapigano hayo kuingia Uganda.

“Hali haijatulia katika mpaka wa Bunagana kwa sababu idadi ya wanajeshi wa FARDC imeongezeka katika sehemu hiyo,” alisema Enanga akiongezea kwamba “wana lengo la kushambulia kambi za waasi hao katika sehemu ya Bunagana lakini maafisa wetu wa usalama wa[o imara mpakani na wanashirikiana na UNHCR, ofisi ya Waziri mkuu na shirika la msalaba mwekundu, miongoni mwa mashirika mengine.”

Nani anaongoza kundi la m23?

Kundi la waasi wa M23 linaogozwa na Gen. Sultan Makenga. Kundi hilo lilikimbilia Uganda kufuatia mashambulizi makali ya wanajeshi wa Afrika kusini, Malawi na Tanzania.

Makenga alirejea DRC mwaka 2017 ambako anaripotiwa kusimamia mashambulizi hayo dhidi ya wanajeshi wa serikali.

Wiki iliyopita, DRC iliishutumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi hao, madai ambayo Rwanda ilipinga vikali.

Uganda ilianzsiha ujenzi wa barabara mashariki mwa DRC kwa lengo la kupanua soko la bidhaa zake na kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

Raia kadhaa wa DRC wanaendelea kukimbilia Uganda kufuatia mapigano hayo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG