Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:06

DRC: Waasi wa M23 watangaza sitisho la muda la mapigano


Wanajeshi wa DRC wanaopambana na waasi wa M23.
Wanajeshi wa DRC wanaopambana na waasi wa M23.

Kundi la waasi la M23 linaloshutumiwa kwa kutekeleza mashambulizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limetangaza kusitisha mapigano, baada ya siku kadhaa za makabiliano makali na jeshi la kitaifa la DRC, msemaji wake amesema kupitia taarifa.

Kundi hilo limesema linataka kufanya mazungumzo na serikali na kwamba limewaondoa wapiganaji wake katika eneo la mapigano, ili kuepusha makabiliano mapya na jeshi la Kongo.

Msemaji wa jeshi la Kongo na msemaji wa serikali hakuweza kupatikana mara moja, kutoa maoni yao, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Mapigano makali yalizuka Jumatatu wiki hii baada ya waasi wa M23 kushambulia maeneo mawili ya jeshi la Kongo karibu na mpaka wa Uganda na Rwanda na kusonga mbele kwenye miji ya karibu, na kusababisha maelfu ya watu kukimbilia nchini Uganda Uganda.

Kundi la M23 liliteka sehemu kubwa wakati wa uasi wa mwaka 2012 na 2013, kabla ya wapiganaji wake kufurushwa na vikosi vya Kongo na Umoja wa Mataifa. Tangu wakati huo, wamerejea kutoka nchi jirani kufanya mashambulizi.

Msemaji wa M23 Willy Ngoma hapo awali alisema kuwa wapiganaji wake walikuwa wakijikinga na kulishutumu jeshi la Kongo kwa kuanzisha vita dhidi yao.

Kumekuwa na juhudi za kikanda katika miaka ya hivi karibuni kuwasambaratisha waasi wa M23, lakini viongozi wake wamelalamikia utekelezwaji polepole wa makubaliano ya amani.

XS
SM
MD
LG