Jeshi la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamedai kwamba waasi wa M23 ndio walitengua ndege hiyo na kusababisha vifo vya wanajeshi sita wa Pakistan, mmoja wa Russia na mwingine wa Serbia.
Ndege hiyo ilianguka katika mkowa wa Kivu kaskazini, ambapo mapigano makali yamekuwa yakiendelea kati ya waashi wa M23 na wanajeshi wa DRC.
Waasi wa M23, ambao walikuwa wamekimbia kutoka DRC mwaka 2013, wamejikusanya na kuchukua udhibithi wa sehemu muhimu nchini DRC tangu jumatatu.
Umoja wa mataifa umesema kwamba zaidi ya watu 13,000 wamekimbia makwao na wengi wako kuingia Uganda kama wakimbizi kutokana na mapigano makali kati ya waasi hao wa M23 na wanajeshi wa serikali.