Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:34

Mkutano wa G7 kuzungumzia janga la moto misitu ya Amazon


Ni takriban masaa 24 kabla ya viongozi wa dunia akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump kuwasili katika mkutano wa mataifa saba matajiri duniani.

Mkutano huo unaofanyika kusini magharibi ya Ufaransa, mji wa mapumziko ambapo viongozi hao watajadiliana tofauti zao katika masuala mbalimbali ikiwemo suala la kuteketea kwa moto misitu ya Amazon na jinsi ya kukabiliana na hali hiyo.

Mabadiliko ya tabia nchi

Vyanzo vya habari nchini Ufaransa vimeripoti kuwa mkutano huo pia utaangazia mabadiliko ya tabia nchi, mgogoro wa Iran na ushuru. Wakati huo huo mji huo uliowapokea viongozi hao, Biarritz, umewekewa ulinzi imara.

Polisi wapatao 13,000 wamepelekwa katika mji huo wa kifahari – ambapo kila polisi mmoja anauwezo wa kukabiliana na watu wawili – ili kuhakikisha usalama na kuzuia vurugu zozote za maandamano dhidi ya utandawazi ambayo yalikuwa yanatarajiwa katika mpaka ulioko karibu na eneo la Ufaransa linalozungumza kihispania.

Serikali inakadiria gharama za mkutano huo zitafikia kiasi cha Euro milioni 36 (dola za Marekani 40 milioni).

Hotel du Palais

Biarritz inajulikana kwa hoteli yake ya kifahari ya Hotel du Palais, iliyojengwa karne ya 19 kama nyumba ya mapumziko kwa ajili ya Malikia Eugenie, makasino ya kamari na michezo mashuhuri ya baharini.

Mwenyeji wa mkutano huo Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa hana matarajio makubwa ya kufikia makubaliano kuepuka kutokea tena matatizo yaliyotokea mwaka 2018 wakati Trump aliposababisha rapsha katika mkutano uliyofanyika Canada kwa kuondoka mkutanoni kabla ya kumalizika na hivyo kutokuwepo tamko la pamoja.

Umoja wa Ulaya

Macron ambaye ni mkereketwa wa Umoja wa Ulaya na matetezi wa ushirikiano wa kimataifa, anamatarajio ya kupiga hatua katika kuwasilisha msimamo wa pamoja, na mkutano huo kuangaza suala pana la kupunguza hali ya kutokuwepo usawa duniani.

Kikundi cha G7 kinajumuisha Marekani, Ufaransa, Uingereza, Japan, Ujerumani, Italia na Canada na Umoja wa Ulaya pia huhudhuria mkutano. Mwaka huu, Macron pia amemkaribisha kiongozi wa Australia, Burkina Faso, Chile, Misri, Senegal, Rwanda na Afrika Kusini kuongeza wigo la mjadala juu ya kukosekana usawa duniani.

XS
SM
MD
LG