Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:36

'Mkutano wa G7 kuangaza ugaidi na Korea Kaskazini'


Rais Donald Trump na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe
Rais Donald Trump na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe

Rais Donald Trump wa Marekani amesema ugaidi na Korea Kaskazini ni masuala yaliyo juu ya agenda ya mkutano wa viongozi wa Kikundi cha nchi Saba (G7) huko Italy.

Viongozi kutoka mataifa makubwa saba wameanza kukutana Ijumaa huko mji wa Sicily, kisiwa kikubwa kuliko vyote katika bahari ya Mediterranean.

Akiwa amekaa pamoja na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, Rais wa Marekani amesema mkutano huo “utaangaza hasa juu ya tatizo la Korea Kaskazini.”

Wakati ugaidi pia utakuwa ni tatizo la msingi litakalo zungumziwa na viongozi hao katika mkutano wao wa siku mbili katika kisiwa hicho cha Italy, Jaribio la Korea Kaskazini la silaha za nyuklia na utengenezaji wa kombora unahusisha “tatizo kubwa, ni tatizo la dunia nzima,” Trump amesema. “Hili litapatiwa suluhu hadi kufikia kiwango fulani. Litatatuliwa, sina shaka.”

Biashara ni eneo jingine kubwa linalofikiriwa na viongozi wenzake Trump ambao wamekusanyika katika fukwe ya mji wa Taormina.

Wanatarajia kumshawishi Trump kubadilisha msimamo wake katika masuala ya biashara na mabadiliko ya tabia nchi.

“Tutakuwa na mazungumzo yenye tija kuhusu biashara na tutazungumzia kuhusu soko huru na la wazi linamaanisha nini,” mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Uchumi, Gary Cohn, amewaambia waandishi akiwa katika ndege ya Air Force One wakati wakielekea Sicily kutoka Belgium.

XS
SM
MD
LG