Uchunguzi umeamriwa ufanyike kufahamu nini hasa kilisababisha mkanyagano huo mapema Jumamosi katika kaburi la Mata Vaishnav Devi, ambako maelfu ya waumini wa kihindu walikusanyika kutoa heshima zao katika mji wa kilimani wa Katra karibu na mji wa kusini wa Jammu.
Mahesh muumini ambaye alijitambulisha kwa jina moja tu, alisema mkanyagano ulitokea karibu na moja ya milango ambako mahujaji waliingia na kutoka katika eneo hilo makaburi.
“Kuna kitu kilitokea karibu na mlango na nilijikuta nimekandamizwa na watu. Nilikosa pumzi na nilifanikiwa kusimama haraka,” alisema. “Niliwaona watu wakipita juu ya miili. Ilikuwa na tukio la kutisha, lakini nilifanikiwa kuwasaidia baadhi ya watu waliojeruhiwa.”
Muumini mwingine Priyansh alisema yeye na rafikji zake 10 kutoka New Delhi waliwasili Ijumma usiku ili kutembelea eneo hilo la makabyuri na kwamba rafiki zake wawili walifariki katika ajali hiyo.
“Sijawahi kuona kitu kama hiki,” alisema.
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi alituma salaam za rambi rambi kupitia ujumbe wake kwa njia ya Twitter.
“Nimesikitishwa san ana vifo vya watu kutokana na mkanyagano,” Modi aliandika.
Mahujaji mara kwa mara wanatembea kwa miguu kuelekea kwenye kilele cha hekalu, ambapo ni moja ya eneo linalotembelewa sana huko kaskazini mwa India.
Mikanyago inayosababisha vifo ni kawaida wakati wa sherehe za kidini nchini India,wakati mikusanyiko mikubwa mara nyingine inafikia mamilioni ya watu, wanakusanyiak katika maeneo madogo kukiwa na hatua chache za kiusalama au kudhibiti msongamano.
Mwaka 2012, mahujaji walitembelea hekalu maarufu kwa sherehe za wahindu katikati mwa India katika jimbo la Madhya Pradesh kulitokea mkanyagano ambao ulisababisha daraja kuvunjika, na takriban watu 115 walikanyagwa hadi kufa au wengine wengi walikufa ndani yam to walikotumbukia.
Zaidi ya waumini 100 wa kihindu walifariki mwaka 2011 katika mkanyagao kwenye sherehe za kidini katika jimbo la kusini mwa India la Kerala.