Maambukizi mapya 366,161 na vifo 3,754 vilivyoripotiwa na Wizara ya Afya, ikipandisha idadi ya maambukizi nchini India hadi milioni 22.66 na vifo 246,116 wakati hospitali nyingi zimepungukiwa na oksijeni na vitanda, na kufurika kwa vyumba vya kuhifadhia maiti.
Majimbo mengi yameweka vikwazo vikali zaidi katika mwezi uliopita, wakati wengine wameweka zuio la shughuli mbalimbali na kufunga kumbi za sinema, migahawa, baa na maduka makubwa.
Lakini shinikizo linazidi kuongezeka kwa Modi kutangaza kufungwa kwa nchi nzima kama alivyofanya wakati wa wimbi la kwanza la maambukizo mwaka 2020.
Anapambana na ukosoaji kwa kuruhusu mikusanyiko mikubwa kwenye sherehe za kidini na kufanya mikutano mikubwa ya uchaguzi, katika miezi miwili iliyopita hata wakati visa vya maambukizi, vilikuwa vikiongezeka.