Maafisa magharibi mwa India wanasema wagonjwa 10 wamefariki dunia baada ya moto kuzuka katika wadi ya hospitali ya COVID-19. Afisa mmoja aliiambia Televisheni ya New Delhi leo Jumamosi kwamba karibu wagonjwa 17 walikuwa katika wadi katika mji wa Ahmed-nagar katika jimbo la Mahara-shtra wakati moto huo ulipozuka.
Wagonjwa waliosalia wamehamishiwa wadi ya wagonjwa wa COVID-katika hospitali nyingine. Wakati moto huo ukiwa umedhibitiwa, chanzo chake hakijafahamika mara moja.
Matukio kama haya si jambo lisilo la kawaida nchini India. Mwezi Mei, wakati nchi hiyo ilipokuwa ikipambana na kuongezeka kwa visa vya ugonjwa wa Covid moto katika wodi ya wagonjwa wa COVID magharibi mwa India uliwaua wagonjwa wasiopungua 18. Matengenezo duni na ukosefu wa vifaa sahihi vya kuzima moto mara nyingi husababisha vifo nchini India.