Katika baadhi ya kambi za watu waliokoseshwa makaazi huko Darfur Kaskazini, wakaazi, madaktari na wafanyakazi wa misaada wanasema watu wamelazimika kula udongo na majani.
Kwa mujibu wa shirika linaloangazia usalama wa chakula, IPC, takriban watu milioni 18 nchini Sudan, zaidi ya theluthi moja ya watu, wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Wakati huo huo zaidi ya watu nusu milioni wanalazimika kuvuka mpaka karibu kila siku na kuingia Sudan Kusini kwa kutumia vivuko mbalimbali vya mpaka.
Idadi ya wanaokimbia inazidi kuongezeka huku mzozo ukiendelea, watu wengi wanafika wakiwa wamedhoofika, njaa na waliokata tamaa.
Wafanykazi wa misaada walioko kwenye eneo hilo wanasema idadi kubwa ya watu wanaowasili kutoka Sudan huingia katika kijiji cha Renk nchini Sudan Kusini kila siku na hii inasababisha changamoto kubwa kwa juhudi za kibinadamu katika kusimamia na kutoa msaada.
Forum