Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 10:57

Wakulima Sudan Kusini wahofia kupoteza soko la mazao yao


Wanawake waliopoteza makazi wakisubiri mgao wa chakula kutoka Mpango wa Chakula Duniani huko Bentiu, South Sudan, Feb. 6, 2023
Wanawake waliopoteza makazi wakisubiri mgao wa chakula kutoka Mpango wa Chakula Duniani huko Bentiu, South Sudan, Feb. 6, 2023

Wakulima wa Sudan Kusini ambao wamekuwa wakiyategemea mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanyakazi nchini humo sasa wanasema wanahofia kupoteza soko lililopo tayari kwa mazao yao, iwapo Umoja wa Mataifa utatekeleza tishio lake la kupunguza operesheni zake katika taifa hilo changa duniani.

Hii imekuja baada ya Marekani, Umoja wa Ulaya na Uingereza kuelezea wasiwasi kuhusu uamuzi wa Juba wa kuweka ushuru katika baadhi ya bidhaa zinazonunuliwa na U.N.

Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kulinda Amani Sudan Kusini — UNMISS — tayari imepunguza operesheni zake za usalama huko Sudan Kusini.

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusin Nicholas Haysom anasema hatua ya Juba kutoka kodi katika huduma mbalimbali zimetolewa na UN huko Sudan Kusini kutasababisha matokeo mabaya yakiwemo kukatwa kwa misaada na uungwaji mkono wa huduma nyingine za kibinadamu.

Katika taarifa ya pamoja ya Marekani, Canada, Umoja wa Ulaya, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Uholanzi, Norway, Sweden, Uswizi na Uingereza wanaishutumu Juba kwa kuweka kodi katika vibali kadhaa na ada, kinyume na utendaji wa kimataifa na sheria za Sudan Kusini.

Hizi ni pamoja na kibali cha uidhinishaji wa E Petroleum, tozo ya forodha, noti ya kielectroniki ya kufuatilia shehena, uchunguzi wa maabara ya mgao wa chakula na ada ya kusindikiza ya usalama.

Forum

XS
SM
MD
LG