"Tunaomba Mwenyezi Mungu hali ya kawaida irejee na kufungua tena mipaka kati ya nchi zetu mbili jirani, na watu wetu ambao ni ndugu," Mohammed VI, mwenye umri wa miaka 59, alisema Jumamosi jioni katika hotuba ya kuadhimisha siku alipoingia mamlakani mnamo mwaka wa 1999.
Mipaka kati ya nchi hizo mbili imekuwa imefungwa tangu mwaka 1994, na kuacha familia zikiwa zimegawanyika baada ya Morocco kumshutumu jirani yake kwa kuhusika na shambulio la wapiganaji wa Kiislamu kwenye hoteli ya Marrakesh, lililosababisha vifo vya watalii wawili, na kupelekea Algeria kufunga mipaka.
Tangu wakati huo, mvutano umeendelea kati ya nchi hizo mbili, ukichochewa na mzozo wao kuhusu Sahara Magharibi, ambapo chama cha Polisario Front, kinachoungwa mkono na Algiers kinatafuta uhuru kutoka kwa utawala wa Rabat na kutangaza eneo hilo kuwa "eneo la vita".
Algeria ilikata uhusiano mnamo Agosti 2021, ikiishutumu Rabat kwa "vitendo vya uhasama", hatua ambayo Morocco ilisema "haikuwa na ukweli wowote".
Forum