Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 15:16

Gambia yawarejesha nyumbani raia wake waliokwama Libya


Wahamiaji kutoka kusini mwa jangwa la Sahara walihudhuria maandamano ya kupinga hali mbaya ya wahamiaji katika mji wa Sfax huko Tunisia tarehe 7 Julai , 2023. Picha na HOUSSEM ZOUARI / AFP.
Wahamiaji kutoka kusini mwa jangwa la Sahara walihudhuria maandamano ya kupinga hali mbaya ya wahamiaji katika mji wa Sfax huko Tunisia tarehe 7 Julai , 2023. Picha na HOUSSEM ZOUARI / AFP.

Serikali ya Gambia imewarejesha nyumbani wahamiaji 296 katika kipindi cha wiki mbili, zaidi ya nusu yao wakiwa wamekwama nchini Libya, wizara ya mambo ya nje ilisema Jumapili.

Raia 140 wa Gambia walirejeshwa nyumbani kati ya mwezi Juni 21 na Julai 4 baada ya maafisa wa Senegal, Mauritania na Morocco kuzuia boti zilizokuwa zimebeba raia wa taifa hilo la Afrika Magharibi, msemaji wa wizara alithibitisha.

Jumla ya raia 231 wa Gambia walikuwa ndani ya boti hizo tatu, wizara ilisema katika taarifa yake, lakini wengi wao "walitoroka" kabla ya kurudishwa.

Wakati huo huo, Wagambia 156 waliokuwa wamekwama Libya walirejeshwa nchini tarehe 24 Juni, ilisema taarifa hiyo ya wizara.

Siku ya Alhamisi, Human Rights Watch iliishutumu Tunisia kwa kuwafukuza mamia ya wahamiaji wa kiafrika wanaotoka nchi za kusini mwa jangwa la Sahara kwenda kwenye eneo la jangwa karibu na mpaka wa Libya tangu Julai 2, kufuatia ghasia dhidi ya wahamiaji katika mji wa Sfax.

"Kuhusiana na video ya kuhuzunisha za wahamiaji nchini Tunisia zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Wizara ya Mambo ya Nje inalifanyia kazi suala hilo kwa karibu... ili kujua idadi yao na kuthibitisha uraia wao kama sehemu ya utaratibu wa kuwahamisha," ilisema taarifa hiyo.

Mapema mwaka huu, mataifa ya Afrika Magharibi yakiwemo Burkina Faso, Guinea, Ivory Coast, Mali na Senegal yaliwarudisha nyumbani mamia ya raia wao waliokuwa Tunisia wakati kukiwa na wimbi la mashambulizi kwa misingi ya ubaguzi.

Hali hii ilifuatia hotuba ndefu, yenye hasira ilyotolewa na rais wa Tunisia akilaumu "makundi ya wahamiaji haramu kutoka kusini mwa jangwa la Sahara" kwa uhalifu na kudai "njama ya uhalifu" ya kubadilisha muundo wa idadi ya watu wa nchi hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG