Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 19:58

Mahakama ya London kuamua kuhusu uhalali wa mpango wa kupeleka wahamiaji Rwanda


Boti iliyobeba wahamiaji
Boti iliyobeba wahamiaji

Mahakama ya rufaa ya London Alhamisi inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa mpango wa Uingereza wa kuwapeleka wakimbizi nchini Rwanda, uamuzi ambao unaweza kuathiri ahadi ya waziri mkuu Rishi Sunak ya kuzuia wahamiaji kuingia nchini humo kwa kutumia boti.

Chini ya mkataba uliyotiwa saini mwaka jana, Uingereza inapanga kupeleka maelfu ya waomba hifadhi wanaowasili kwenye fukwe zake hadi Rwanda, ambalo ni taifa la mashariki mwa Afrika lililo umbali wa zaidi ya kilomita 6,400 kutoka London.

Ndege ya kwanza iliyokuwa imejaa wahamiaji alizuiliwa kuondoka dadika za mwisho mwaka mmoja uliyopita na mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu ECHR, ambayo ilisimamisha mchakato mzima hadi pale suluhisho la kisheria lingepatikana nchini Uingereza.

Mwezi Desemba mwaka jana, mahakama kuu mjini London aliamua kwamba mpango huo ulikuwa halali, lakini ulikuwa ikipingwa na waomba hifadhi kutoka mataifa mbalimbali, pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Iwapo serikali itashinda kesi hiyo, haina maana kwamba ndege za wahamiaji zitaanza kuruka mara moja, kutokana na kuwa huenda kukawa na kesi nyingine za rufaa.

Kando na hilo uamuzi wa ECHR unazuia upelekazi wa wahamiaji nje ya Uingereza hadi baada ya wiki tatu tangu kumalizika kwa kesi. Iwapo majaji wataamua kuwa mpango huo ni halali, basi ndege za wahamiaji huenda zikaanza kuruka baadaye mwaka huu.

Waziri Mkuu Sunak anaona mpango huo ukiwa mbinu muafaka ya kuvunja moyo wahamiaji wanaowasili Ulaya kupitia baharini. Kuzuia boti za wahamiaji ni moja wapo ya vipaumbele vyake, akiamini kuwa hatua hiyo itatoa ushindi kwa chama chake cha Konsavative kwenye uchaguzi ujao.

Forum

XS
SM
MD
LG