Kyriakos Mitsotakis, muhula wa pili madarakani.
Uchaguzi wa Jumapili unafanyika chini ya kivuli cha ajali ya meli ya wahamiaji ya Juni 14 ambapo mamia ya watu wanahofiwa kupoteza maisha kusini mwa Ugiriki.
Moja ya maafa makubwa kama haya kwa miaka, imeonyesha mgawanyiko miongoni mwa vyama kuhusiana na uhamiaji.
Chama cha New Democracy cha Mitsotakis, kilishinda uchaguzi wa Mei 21, kikiwa na pointi 20 mbele ya chama cha mrengo wa kushoto cha Syriza kilichotawala Ugiriki kuanzia 2015 - 2019.
Lakini haikufikia idadi kubwa ya waliohitajika kutawala bila kuunda muungano, na hivyo kusababisha duru ya pili ya kura chini ya kanuni tofauti zinazorahisisha chama kilichoshinda kupata wingi wa viti katika bunge lenye viti 300.
Forum