Kituo cha Uratibu wa Pamoja, chombo kilichoundwa chini ya Juhudi ya Nafaka ya Black Sea kufuatilia utekelezaji wake, kimeidhinisha meli hizo kuondoka kupitia njia za baharini ya kibinadamu.
Meli hizo zilizoondoka kwenye bandari za Ukraine zinaelekea China, Italia na maeneo mawili nchini Uturuki.
Meli ya tano imeidhinishwa kuingia Ukraine kuchukua mizigo.
Ukraine ni moja ya wazalishaji wa chakula wa ulimwenguni na vizuizi kwenye bandari zake vimepelekea kupanda kwa bei ya vyakula duniani na kutishia kuzuka kwa njaa.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, katika hotuba yake ya kila siku Jumamosi amelaani “ukimya wa wazi” ulioonyeshwa na Shirika la Amnesty International kwa kushindwa kutoa kauli dhidi ya shambulizi la Russia huko Zaporizhzhia NPP, kiwanda cha umeme ambacho ni kinu cha kikubwa sana cha nishati ya nyuklia Ulaya.
Ukimya huo, Zelenskyy amesema, “unaonyesha namna taasisi hiyo ilivyokuwa inachagua kile cha kusema kujiridhisha yenyewe.
Mkuu wa Shirika la kimataifa la Nishati ya Atomiki alitoa kauli juu ya hali ya kinu cha nishati ya nyuklia katika taarifa yake Jumamosi, akisema, “Shambulizi la kijeshi linahatarisha usalama na ulinzi wa kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzya ni jambo lisilokubalika hata kidogo na lazima liepukwe kwa namna yoyote ile.