Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 02:55

Russia na Marekani zasema ziko tayari kujadili suala la kubadilishana wafungwa


Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu raia wa Marekani Brittney Griner aliyepewa kifungo cha miaka tisa na mahakama ya Russia.
Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu raia wa Marekani Brittney Griner aliyepewa kifungo cha miaka tisa na mahakama ya Russia.

Russia na Marekani zimesema leo Ijumaa kwamba ziko tayari kujadili suala la kubadilishana wafungwa, siku moja baada ya mahakama ya Russia kumhukumu nyota wa mpira wa vikapu, Brittney Griner, kifungo cha miaka tisa gerezani, kwa kosa linalohusiana na matumizi ya dawa za kulevya.

Kesi dhidi ya Griner, mshindi wa medali ya dhahabu mara mbili ya Olimpiki na nyota wa Chama cha Kikapu cha Kitaifa cha Wanawake (WNBA), ilimtumbukiza kwenye mtafaruku wa kisiasa, baada ya Russia kutuma wanajeshi nchini Ukraine mwezi Februari mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov alisema Rais Vladimir Putin, na mwenzake wa Marekani Joe Biden walikuwa wamekubaliana hapo awali, kuhusu njia ya kidiplomasia, ambayo inapaswa kutumika kujadili uwezekano wa kubadilishana wafungwa.

"Tuko tayari kujadili mada hii, lakini ndani ya mfumo na njia ambayo ilikubaliwa na marais Putin na Biden," Lavrov alisema wakati wa ziara yake nchini Kambodia.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema Washington iko tayari kushirikiana na Moscow kupitia njia za kidiplomasia zilizowekwa.

Alisema hukumu ya Griner ilikuwa ni mwenelezo wa ukiukaji wa haki zake, baada ya kuzuiliwa kimakosa, na Russia na kuzidisha dhuluma ambayo alikuwa ametendewa.

XS
SM
MD
LG