Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 07, 2025 Local time: 00:43

Mjumbe wa Marekani kwenye UN afanya ziara ya Afrika


Mjumbe wa Marekani kwenye UN, Thomas Greenfield
Mjumbe wa Marekani kwenye UN, Thomas Greenfield

Mjumbe wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Alhamisi ameanza ziara yake barani Afrika, akisema kwamba madhumuni yake ni kutadhmini namna Marekani inavyoweza kusaidia Uganda, Ghana na Cape Verde kukabiliana na uhaba wa chakula.

Hali hiyo imeendelea kushuhudiwa kwenye mataifa mengi ya Afrika katika miezi ya karibuni, wakati mjumbe huyo akisema kwamba ziara yake haifayiki kwa ajili ya kushindana na Russia na China.

Linda Thomas Greenfield amesema kwamba ziara yake iliyopangwa siku nyingi siyo sehemu ya ushindani ulioko kati ya Marekani na mataifa mengine, lakini ni sehemu ya Marekani ya kuimarisha ushirikiano na viongozi wa Afrika pamoja na watu wake.

Shirika la habari la AP limeripoti kwamba ziara ya Greenfield itakayomalizika Jumapili, itafuatiwa kwa karibu na ile ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kwenye mataifa ya Afrika Kusini, Congo na Rwanda wiki ijayo.

Ziara za maafisa hao wa ngazi ya juu wa Marekani zimekuja muda mfupi baada ya waziri wa mambo ya kigeni wa Russia Sergei Lavrov kuzuru mataifa ya Misri, Ethiopia, Uganda pamoja na DRC wiki moja iliyopita, wakati akilaumu Marekani pamoja na mataifa mengine ya Ulaya kutokana na ongezeko la bei za vyakula linaloshuhudiwa ulimwenguni.

XS
SM
MD
LG