Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:49

Russia yaanza mashambulizi mapya mashariki mwa Ukraine


Mkazi wa eneo akiwa na baiskeli yake huko Bakhmut, mashariki mwa Ukraine, Aug. 4, 2022, wakati Russian ikiendeleza uvamizi wa Ukraine.
Mkazi wa eneo akiwa na baiskeli yake huko Bakhmut, mashariki mwa Ukraine, Aug. 4, 2022, wakati Russian ikiendeleza uvamizi wa Ukraine.

Wakati Russia imeanza mashambulizi Jumamosi katika miji miwili muhimu huko Mashariki mwa Ukraine, chombo ambacho kinafuatilia  meli zinaoingia na kutoka  katika bandari za Ukraine kimeidhinisha meli tano zaidi kuanza safari zake.

Meli nne zimepangwa kuondoka Jumapili na takriban tani 162,000 za vyakula.

Majeshi ya Russia Jumamosi yalianza kufanya mashambulizi katika miji ya kimkakati ya Bakhmut na Avdiivka katika mkoa wa Donetsk Mashariki mwa Ukraine, kwa mujibu wa majeshi ya Ukraine na maafisa wa eneo.

Bakhmut and Avdiivka are prime targets for Russia; analysts say Moscow must take Bakhmut in order to advance on the key regional hubs of Sloviansk and Kramatorsk.

Bakhmut na Avdiivka ni malengo mawili muhimu kwa Russia; wachambuzi wanasema Moscow lazima waiteke Bakhmut ili kuweza kusonga mbele katika vituo muhimu vya kieneo vya Sloviansk na Kramatorsk.

Raia watano waliuawa, akiwemo mmoja huko Avdiivka, na wengine 14 walijeruhiwa kufuatia mashambulizi ya Russia katika mkoa wa Donetsk. Gavana wa Donetsk Pavlo Kyrylenko ameandika katika ujumbe wa Telegram Jumamosi.

Mara ya mwisho Russia ilishambulia Sloviansk Julai 30, lakini majeshi ya Ukraine yanaimarisha nafasi zao kuzunguka mji wa kimkakati wa mashariki kabla ya mashambulizi mapya yanayotarajiwa kufanywa na Russia.

Sloviansk ni eneo la mkakati katika utashi wa Moscow wa kuuteka mkoa mzima wa Donetsk, ambapo wengi wanazungumza lugha ya kirusi katika eneo la mashariki mwa Ukraine.

Majeshi ya Russia na vikundi vinavyoungwa mkono na Moscow wanadhibiti asilimia 60 ya jimbo hilo.

XS
SM
MD
LG