Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 18:39

Shambulizi la kituo cha umeme: Ukraine na Russia zatupiana lawama


kituo cha umeme cha Zaporizhzhia nchini Ukraine, kiwanda kikubwa sana cha  nishati ya nyuklia Ulaya katika mkoa wa Zaporizhzhia, Ukraine, Aug. 4, 2022.
kituo cha umeme cha Zaporizhzhia nchini Ukraine, kiwanda kikubwa sana cha  nishati ya nyuklia Ulaya katika mkoa wa Zaporizhzhia, Ukraine, Aug. 4, 2022.

Ukraine na Russia zimelaumiana Ijumaa kwa shambulizi ambalo lilipiga kituo cha umeme cha Zaporizhzhia nchini Ukraine, kiwanda kikubwa sana cha nishati ya nyuklia Ulaya.

“Mashambulizi matatu yalirekodiwa katika eneo la kituo hicho, karibu na moja ya vinu vya kuzalisha umeme ambako kituo hicho cha nyuklia kipo,” Energoatom, kampuni ya taifa ya nishati ya nyuklia ya Ukraine imesema katika taarifa yake.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema majeshi ya Ukraine yanahusika na uharibifu wa kituo hicho. “Majeshi ya Ukraine yalifanya mashambulizi matatu ya makombora katika eneo hilo la kiwanda cha nishati ya nyuklia huko Zaporizhzhia na mji wa Enerhodar,” wizara ilisema katika taarifa yake.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya kila siku jana Ijumaa kuwa shambulizi lililofanywa na Russia katika kiwanda cha nyuklia “ siyo hoja pekee ya kupendelea kuitambua Russia kama taifa linalofadhili ugaidi” na “ni hoja ya kupitisha vikwazo vikali dhidi ya sekta nzima ya nyuklia ya Russia.”

Energoatom ilisema kulikuwa hakuna dalili kuwa uharibifu huo ulisababisha kuvuja kwa miale ya nyuklia.

Mashambulizi matatu

Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema majeshi ya Ukraine yalikuwa yanahusika na uharibifu wa kiwanda hicho.

“Majeshi ya Ukraine yalifanya mashambulizi matatu ya makombora katika eneo la kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia na mji wa Enerhodar,” wizara hiyo ilisema katika taarifa yake.

“Bahati nzuri, shambulizi lililofanywa na Ukraine halikupiga eneo la kiwanda cha mafuta na kiwanda cha Oxygen kilicho karibu, na kuepusha moto mkubwa na uwezekano wa kuvuja kwa miale ya nyuklia,” ilisema.

Wanajeshi wa Russia wamevamia mtambo huo huko Kusini mwa Ukraine tangu mwezi Machi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken Jumatatu ameishutumu Russia kwa kutumia kiwanda hicho kama ngao yake kwa majeshi yake.

XS
SM
MD
LG