Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:06

Marekani yaishtaki kampuni ya SpaceX kwa "kuwabagua wakimbizi na waomba hifadhi"


SpaceX
SpaceX

Idara ya Sheria ya Marekani inaishtaki SpaceX, inayomilikiwa na bilionea Elon Musk kwa kukataa kuajiri wakimbizi na wanaotafuta hifadhi katika kampuni hiyo ya roketi.

Katika kesi iliyowasilishwa Alhamisi, Idara hiyo ilisema SpaceX ilibagua mara kwa mara waombaji kazi hao kati ya mwaka 2018 na 2022, kinyume na sheria za uhamiaji za Marekani.

Mashtaka hayo yanaeleza kwamba Musk na maafisa wengine wa SpaceX, walidai kwa uwongo, kwamba kampuni hiyo iliruhusiwa tu kuajiri raia wa Marekani, na wakaazi wa kudumu, kutokana na sheria za udhibiti wa usafirishaji bidhaa zinazoratibu uhamishaji wa teknolojia nyeti.

Idara ya Sheria ya sheria inasema kwamba sheria za udhibiti wa usafirishaji wa Marekni haziweke vizuizi kama hivyo,.

Sheria hizo zinazuia uhamishaji wa teknolojia nyeti kwa mashirika ya kigeni, lakini hazizuii kampuni za teknolojia ya juu kama vile SpaceX kuajiri waombaji kazi ambao wamepewa hadhi ya ukimbizi au hifadhi nchini Marekani.

Raia wa kigeni, hata hivyo, wanahitaji kibali maalum.

Kampuni hiyo haikujibu ombi la VOA la kutoa maoni kuhusu kesi hiyo na iwapo ilikuwa imebadilisha sera yake ya uajiri.

Kitengo cha haki za kiraia cha Idara ya sheria ya Marekani kilianzisha uchunguzi kuhusu SpaceX mnamo mwaka 2020, baada ya kupokea madai ya mazoea ya kuajiri ya kibaguzi ya kampuni.

Forum

XS
SM
MD
LG