Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:27

Setilaiti ya kwanza inayofanya kazi Kenya ilirushwa Jumamosi kutoka Marekani


Baadhi ya wapiga picha wakishuhudia kurushwa kwa roketi ya SpaceX Falcon 9
Baadhi ya wapiga picha wakishuhudia kurushwa kwa roketi ya SpaceX Falcon 9

Uzinduzi awali ulipangwa kufanyika Jumatatu Marekani uliahirishwa kutokana na hali mbaya ya hewa. Jumamosi roketi ya SpaceX Falcon-9 iliruka saa kumi na mbili na dakika 48 asubuhi kutoka Vandenberg jimbo la California kabla ya kupeleka satelaiti kadhaa saa moja baadaye ikijumuisha Taifa la Kenya-1

Setilaiti ya kwanza inayofanya kazi nchini Kenya ilirushwa angani Jumamosi na roketi ya SpaceX iliyoruka kutoka California nchini Marekani kulingana na picha kutoka kwa kampuni ya anga za juu ya Marekani.

Uzinduzi huo ambao awali ulipangwa kufanyika Jumatatu usiku nchini Marekani uliahirishwa mara kadhaa wiki hii kutokana na hali mbaya ya hewa. Jumamosi roketi ya SpaceX Falcon-9 iliruka saa kumi na mbili na dakika 48 asubuhi kutoka kambi ya Vandenberg kwenye jimbo la California kabla ya kupeleka satelaiti kadhaa saa moja baadaye ikijumuisha Taifa la Kenya-1.

Satelaiti hiyo iliyoundwa na kutengenezwa na timu ya watafiti wa Kenya inalenga kutoa takwimu za kilimo na ufuatiliaji wa mazingira nchini Kenya suala linalohitajika sana katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambayo kwa sasa inakabiliwa na ukame wa kihistoria.

Katika taarifa ya pamoja wiki iliyopita Wizara ya Ulinzi ya Kenya na Shirika la Anga za Juu la Kenya (KSA) zilitaja hatua muhimu ambazo zinapaswa kuimarisha uchumi wa anga za juu wa Kenya.

XS
SM
MD
LG