Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:09

Kampuni ya SpaceX kupeleka timu ya wanananga kwenye  Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu

Wanaanga wa NASA Stephen Bowen na Warren "Woody" Hoburg, na Sultan Al-Neyadi wa UAE na mwana anga wa Russia Andrey Fedyaev kabla ya uzinduzi wa timu ya NASA ya SpaceX Crew-6 kutoka Kituo cha Anga cha Kennedy huko Cape Canaveral, Florida, Marekani, Februari. 26, 2023. REUTERS

Kampuni ya roketi ya Elon Musk ya SpaceX ilitarajiwa kuzindua mapema Jumatatu timu inayofuata itakayokuwa ya muda mrefu ya Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

Kampuni ya roketi ya Elon Musk ya SpaceX yazindua timu mapema Jumatatu inayofuata itakayokuwa ya muda mrefu kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu katika obiti, huku mwana anga kutoka Falme za Kiarabu na mwingine wa Russia wakiungana na wafanyakazi wawili wa NASA kwa ajili ya safari hiyo.

Eneo la kuruka SpaceX, linalojumuisha roketi ya Falcon 9 iliyo na chombo kinachofanya kazi kwa kujitegemea cha Crew Dragon kiitwacho Endeavour, kilitarajiwa kuruka saa 7:45 usiku saa za mashariki kutoka Kituo cha Anga cha NASA cha Kennedy huko Cape Canaveral, Florida.

Wafanyakazi hao wanne wanapaswa kufika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) kiasi cha saa 25 baadaye, Jumanne asubuhi, ili kuanza kazi ya miezi sita ya kwenye eneo la nguvu za mvutano za dunia kwenye obit kiasi cha umbali wa maili 250 juu ya Dunia.

XS
SM
MD
LG