Maporomoko ya udongo yalitokea Jumapili usiku karibu na mji wa Kamituga katika jimbo la Kivu Kusini, kwa mujibu wa naibu meya Alexandre Ngandu Kamundala.
Watu wapatao 25, wengi wao wachimba madini, walikuwa wakijihifadhi na mvua katika kibanda wakati maporomoko ya ardhi yalipowakumba, yaliwazoa na kuwapeleka katika mto ambao maji yalikuwa yanakwenda kwa kasi, kamundala alisema.
“watu watano waliweza kuokolewa kwa shida na wengine 20 walichukuliwa na maji. Miili ya watu wanne waliokufa ilipatikana,” alisema Kamundala.
Juhudi za msako na uokoaji zinaendelea kuwatafuta waliopotea. Mwaka 2020, takriban watu 30 katika mji huo huo wa Kamituga walifariki kiatika maporomoko ya ardhi ambayo yalipiga eneo la machimbo ya dhahabu.
Ajali mbaya zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika migodi isiyodhibitiwa nchini Congo, ambapo vifo vingine vinatokea bila kuripotiwa kutoka na migodi hiyo kuwepo katika maeneo yalojitenga kwenye milima na misitu.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AP
Forum