Wapiga kura wengi katika taifa hilo walijitahidi kupiga kura zaidi huko kukiwa na matatizo ya vifaa na changamoto za kiusalama.
Vituo vya kupiga kura nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambavyo havikufunguliwa Jumatano vitafunguliwa Alhamisi, Danis Kadima, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi amesema kupitia kituo kimoja cha redio nchini humo.
Takriba watu milioni 44, karibu nusu ya idadi ya watu wa DRC, walitarajiwa kupiga kura, lakini wengi ikijumuisha watu milioni saba waliokimbia makazi yao kwa sababu ya migogoro katika eneo la mashariki mwa nchi, wamejikuta katika wakati mgumu wa kushiriki kupiga kura.
Mapigano yamewazuia watu milioni 1.5 kutojiandikisha kupiga kura.
Rais wa sasa Felix Tshisekedi, anagombea muhula wake wa pili wa miaka mitano ijayo, akishindana na wagombea wengine 26.
Forum