Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 08:53

Viongozi wa Upinzani DRC kuitisha maandamano ya kulalamikia Uchaguzi


Wafuasi wa Rais wa DRC Felix Tshisekedi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni Desemba 18 mjini Kinshasa.
Wafuasi wa Rais wa DRC Felix Tshisekedi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni Desemba 18 mjini Kinshasa.

Kundi la wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi wa Congo limeandika barua kwa gavana wa Kinshasa likielezea nia ya kuitisha maandamano wiki ijayo, ili kulalamikia uchaguzi wa rais uliozua utata.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, baadhi ya wagombea hao wanadai kuwa kucheleweshwa kwa uchaguzi wa Jumatano huenda kukapelekea udanganyifu, pamoja na kushuka kwa hadhi ya zoezi hilo.

Mara nyingi mivutano ya uchaguzi hupelekea ghasia nchini Congo, kukiwa na hatari ya kuyumba kwa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa madini, na ambalo tayari linakabiliwa na umasikini mkubwa, pamoja na ukosefu wa usalama upande wa mashariki.

Wagombea watano wa upinzani wanapanga kuitisha maandamano ya Decemba 27, kulingana na barua ya Desemba 22 kwa gavana wa Kinshasa, iliyowekwa kwenye ukurasa wa X, na Jean-Marc Kabunda ambaye ni mwakilishi wa mmoja wa wagombea wa urais Martin Fayulu.

“Tutalalamikia dosari zilizojitokeza wakati wa kupiga kura na hata kabla. Pia tutalalamikia kucheleweshwa kwa zoezi hilo,” imeongeza barua hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG