Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:28

Makubaliano ya kihistoria yafikiwa baina ya pande hasimu Sudan


Jenerali Abdel Fattah al-Burhan
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan

Viongozi wa serikali ya mpito nchini Sudan na wakuu wa makundi ya waasi katika jimbo la Darfur leo wamefikia makubaliano ya kihistoria ya mkataba wa amani unaoelezewa ni hatua muhimu ya kwanza kuelekea katika kumaliza vita vya takriban miaka 17.

Kupatikana kwa amani na waasi ni hatua muhimu sana kwa serikali ya mpito ya Sudan ambayo imeingia madarakani miezi kadhaa baada ya kuuangusha utawala wa Bashir April 2019.

Viongozi wa muungano wa makundi ya waasi, Sudan Revolutionary Front (SRF) kutoka jimbo la magharibi la Darfur na majimbo ya kusini ya Kordofan Kusini na Blue Nile waliinua juu mikono yao kama njia ya kusherekea kupatikana kwa mkataba huo.

Wananchi waliolazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita Darfur, wakiwa katika kambi ya wakimbizi.
Wananchi waliolazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita Darfur, wakiwa katika kambi ya wakimbizi.

Mkataba huo ulipendekezwa awali lakini haukusainiwa kama njia ya kuacha mlango wazi kwa makundi mawili muhimu ya waasi kujiunga kwenye makubaliano ya mwisho, maafisa wamesema.

Makundi mawili ya waasi yalikataa kushiriki katika makubaliano hayo.

Wakiwa na hamasa kubwa kusheherekea mafanikio tangu kuangushwa kwa dikteta wa muda mrefu Omar al Bashir mwaka 2019 na kuundwa serikali ya mpito, viongozi wa Sudan walikutana katika mji mkuu wa Sudan kusini wa Juba.

Kusukuma mbele amani na waasi limekuwa suala lililopewa kipaumbele na serikali ya mpito ilioingia madarakani baada ya kuangushwa utawala wa Bashir mwezi April mwaka 2019.

Serikali ya Sudan inayoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan, mkuu wa baraza la utawala na upande wa raia ukiongozwa na waziri mkuu Abdalla Hamdok, inasema inaona ujenzi wa amani kama msingi wamuhimu sana katika juhudi zake zote.

Burhan na Hamdok walihudhuria sherehe za kupatikana mkataba huo, shirika la habari la AFP limeripoti, naye rais wa Sudan kusini Salva Kiir amesimamia sherehe hizo.

Makundi ya waasi ya Sudan kwa kiasi kikubwa yanaundwa na makundi ya waliowachache wasiokuwa Waarabu, ambao kwa muda mrefu walipinga utawala wa Waarabu waliowengi katika serikali ya Khartoum.

Umoja wa Mataifa (UN) unasema takriban watu laki 3 waliuawa huko Darfur tangu waasi walipoamua kuchukua silaha mwaka 2003.

Mzozo katika jimbo la Kordofan Kusini na jimbo la Blue Nile ulizuka mwaka 2011, baada ya Sudan kusini kujipatia uhuru, na hivyo kuanzisha tena vita vya miongo miwili.

Mkataba uliofikiwa Jumatatu unazingatia masuala makuu ya usalama, umiliki wa ardhi, mfumo wa mpito wa sheria, kushirikiana madaraka, na kurejea nyumbani kwa watu waliohama makazi yao kwa sababu ya mapigano.

Pia unapendekeza kuvunjwa kwa makundi ya waasi na kushirikisha wapiganaji wao kwenye jeshi la taifa.

Waasi wa kundi la Sudan Liberation Movement ( SLM) na wale wa kundi la Sudan People’s Liberation Movement North (SPLM-N), waliingia mkataba na serikali Jumamosi.

Lakini kikundi cha SLM kinachoongozwa na Abdelawid Nour na tawi la SPLM-N linaongozwa na Abdelaziz al-Hilu, vilikataa kujiunga kwenye mkataba huo.

Imetayarishwa na mwandishi ketu, Patrick Nduwimana, Washington,DC

XS
SM
MD
LG