Katika hotuba yake ya taifa kwa njia ya televisheni, Rais Kiir alitoa wito kwa Wasudan kusini wote kufanya juhudi za kiuleta amani na maridhiano ya kijamii, akisema kuwa jamii nyingi zimegawanyika kutokana na vita.
"Ghasia za kisiasa hivi sasa hazipo. Kwa bahati mbaya, mafanikio yetu katika kumaliza ghasia za kisiasa hivi sasa yanatishiwa na aina tofauti ya ghasia," alisema Kiir.
"Mzozo wa ndani kwa ndani unaendelea katika maeneo tofauti ya nchi yetu. Kama serikali hatutaruhusu jambo kama hili kujirudia," aliongeza.
Mkuu wa ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, David Shearer aliiambia VOA kwamba watu wapatao mia moja walikufa mwezi uliopita katika wimbi la mashambulizi na mashambulizi ya kujibizana katika jimbo la Jonglei.
-Imetayarishwa na Mkamiti Kibayasi, VOA, Washington DC