Katika kesi hiyo ambayo Nondo alikuwa akikabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kutekwa na kutoa taarifa za uongo, mahakama hiyo imemkuta hana hatia baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kueleza mshitakiwa alifikaje Mafinga.
Shirika la habari la Global Publishers aidha limeripoti kuwa mahakama imesema hakuna ushahidi kutoka upande wa Jamhuri kuwa mshitakiwa alikuwa wapi wakati wa tukio na kuifanya kesi hiyo ikose ushahidi.
Kwa mujibu wa upande wa utetezi imebainika kuwa upande wa mashtaka wametoa ushahidi wa hisia na hivyo mahakama kuamua kumuachia huru.