Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:11

Mahakama yaamuru aliyeuwa wanawake Kenya awekwe kizuizini


Mtuhumiwa wa Mauaji wa yanawake 42, Collins Jumaisi Khalusha (wakwanza kulia aliyesimama) Picha na AFP.
Mtuhumiwa wa Mauaji wa yanawake 42, Collins Jumaisi Khalusha (wakwanza kulia aliyesimama) Picha na AFP.

Mahakma mmoja mjini Nairobi imeamrisha mtuhumiwa mkuu wa ambaye polisi inasema amekiri kuwakatakata na kuwauwa wanawake 42 awekwe kizuizini kwa siku 30 wakati uchunguzi ukiendelea.

Collins Jumaisi Khalusha mwenye umri wa miaka 33 anaelezwa na polisi kuwa kama “shetani” alikamatwa Jumatatu alfajiri, baada ya kugunduliwa kwa miili iliyokatwa na kutupwa katika jalala la taka huko Nairobi.

Tangu siku ya Ijumaa miili 10 ya wanawake iliyochinjwa na kuwekwa ndani ya magunia ya plastiki ilianza kujitokeza katika eneo la kutupa taka katika kitongoji cha Mukuru kulingana na tume ya kitaifa ya haki za binadam na kuzusha hofu miongoni mwa raia.

Mkuu wa idara ya upelelezi wa jinai Mohamed Amin aliwambia waandishi habari Jumatatu kuwa Khalusha alikiri kuwauwa wanawake 42 pamoja na mkewe tangu mwaka 2022. Hajatoa ushahidi wowote kuthibitisha madai hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG