Maafisa wametangaza hali ya dharura katika majimbo sita yaliyoathiriwa vibaya nchini humo.
Ofisi ya umoja wa mataifa inayoratibu maswala ya kibinadamu jumatano ilisema takriban watu zaidi ya laki mbili wameathiriwa na mafuriko kwenye majimbo 15 kati ya 18.
Mwaka jana mvua za vipindi nchini sudan zilizababisha vifo vya watu 80 na kupelekea maelfu ya nyumba kufunikwa na maji.
Wakati huo huo mwaka 2020 karibu watu laki nane waliathiriwa na mafuriko , na kusababisha Sudan kutangaza hali ya dharura.