Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 17:02

Serikali ya mpito ya Sudan Kusini kubaki madarakani kwa miaka miwili zaidi


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ( kushoto) na naibu wake Riek Machar
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ( kushoto) na naibu wake Riek Machar

Viongozi wa  Sudan Kusini Alhamisi wamesema kwamba serikali itabaki madarakani kwa miaka miwili zaidi, ili kukamilisha mageuzi ya kisiasa, kiusalama na uchaguzi, yanayohitajika ili kusogeza taifa mbele.

Waziri wa masuala ya baraza la mawaziri Martin Elia Lomuro wakati wa kufanya tangazo hilo amesema kwamba uamuzi huo imefikiwa ili kukabiliana na changamoto zinazohujumu utekelezwaji wa mkataba wa amani wa 2018, uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochukua miaka minne na nusu, na kuuwa takriban watu laki nne.

Tangazo hilo huenda likakera jumuia ya kimataifa ambayo imelalamikia utawala wa Sudan kusini kwa kushidwa kumaliza kipindi cha mpito kilichoanza Februari 2020. Mkataba wa 2018 unaitisha marekebisho kwa masuala ya kiusalama, mahakama, katiba pamoja na uchaguzi kwenye taifa hilo changa zaidi ulimwenguni.

Wataalam wanasema kwamba utawala ulioko umezembea katika kutekeleza wa marekebisho yanayohitajika. Serikali hiyo inayoongozwa na rais Salva Kiir na naibu wake Riek Machar iliahirisha uchaguzi mkuu uliokuwa ufanyike mwaka ujao kwa kigezo cha kutokuwa na katiba ya kudumu nchini humo.

XS
SM
MD
LG