Ethiopia imesema mtambo wa pili kwenye bwawa lake la kuzalisha umeme ambalo limekumbwa na utata kwenye mto Blue Nile umeanza kufanya kazi.
Bwawa hilo kubwa lililogharimu kiasi cha dola bilioni 4, limesababisha mgogoro mkubwa kati ya nchi hiyo, Misri na Sudan ambazo zinategemea sana maji yam to Nile.
Bwawa hilo linatarajiwa kuzalisha zaidi ya megawati 5000 za umeme litakapokamilika.
Licha ya mazungumzo ya mara kwa mara, hakuna makubaliano yamefikiwa kati ya nchi hizo tatu.
Cairo na Khartoum zinataka makubaliano juu ya matumizi ya maji ya mto Nile na namna ya kukabiliana na ukame endapo utataokea. Nchi hizo pia zimekasirishwa na Ethiopiakwa vile ilianza kujaza maji kwenye bwawa hilo kabla ya makubaliano kufikiwa.
Ethiopia ilianza kuzalisha umeme kutoka kwenye bwawa hilo mwezi Febrauri mwaka huu.
Ujenzi wake ulichukua zaidi ya mwongo mmoja.