Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini umesema katika ripoti yake kwamba kuna ongezeko la asilimia 218 ya visa vya ubakaji na ubakaji unaofanywa na magenge ya watu.
Visa vingi vimeripotiwa kati ya mwezi April na June mwaka 2022.
Mkuu wa ujumbe huo Nicholas Haysom amesema kwamba dhuluma za kimapenzi zimeongezeka sana na zinaathiri maisha ya wanawake na wasichana, akiongezea kwamba jambo hilo haliwezi kukubaliwa kuendelea.
Mapigano kati ya jamii yameendelea kuathiri maisha ya watu wengi nchini Sudan kusini. Mapigano hayo yanaripotiwa kuchochewa na makundi ya wapiganaji yanayoungwa mkono na jeshi la serikali.