Mratibu wa kazi za kikosi cha Polisi cha Umoja wa Afrika, Somalia, AMISOM, Daniel Ali Gwambal amesema maafisa 30 watatumika chini ya kikosi hicho kwa muda wa mwaka mmoja.
Maafisa hao watapelekwa Beletweyne katika jimbo la HirShabelle wakati waliobaki watatumikia nyadhifa mbali mbali katika mji mkuu wa Mogadishu.
Gwambal anasema miongoni mwa kazi ambazo maafisa hao watafanya ni kuwapatia ulinzi wageni wa heshima pamoja na kusaidia idara za usalama, kutoa mafunzo na kusaidia kikosi cha polisi cha Somalia kusimamia usalama wa raia na kupiga doria za pamoja.
Ofisi ya AU inasema kuwasili kwa kundi hilo ni hatua muhimu ya kuimarisha juhudi za utekelezaji sheria na usalama, kwa vile watafanya kazi kwa ushirikiano na wenzao wa somalia kuhakikisha usalama umaimarika katika maeneo yaliyokombolewa.