Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:20

Lviv: Kombora la Russia lapiga jengo la makazi ya watu magharibi mwa Ukraine


Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wakiwa katika eneo la jengo la makazi ya watu lililopigwa na kombora la shambulizi la Russia huko Ukraine, eneo la Lviv, Ukraine Julai 6, 2023.
Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wakiwa katika eneo la jengo la makazi ya watu lililopigwa na kombora la shambulizi la Russia huko Ukraine, eneo la Lviv, Ukraine Julai 6, 2023.

Kombora la Russia limepiga jengo la makazi ya watu huko magharibi mwa Ukraine katika mji wa Lviv siku ya  Alhamisi, limeua watu wasiopungua wanne na kujeruhi wengine tisa.

Meya wa Lviv Andriy Sadovyi alisema kombora hilo pia liliharibu takriban nyumba 60 na magari 50. Sadovyi alilielezea shambulizi hilo kuwa ni kubwa kabisa dhidi ya miundombinu ya ya raia tangu uvamizi wa Russia kuanza mwaka 2022.

“Bila shaka kutakuwa na majibu kwa adui. Ambaye yupo bado,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika ujumbe wake wa Telegram.

Lviv iko karibu na mpaka wa Poland, mbali kutoka maeneo ya mstari wa mbele huko mashariki na kusini mwa Ukraine ambayo yamekabiliwa na mapigano hivi karibuni kati ya majeshi ya Ukraine na Russia.

Ukraine yajibu mashambulizi

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CNN Jumatano, Zelenskyy alisema anataka kuanzisha mashambulizi mapema, lakini muda huo utategemea na upatikanaji wa misaada ya kijeshi kutoka kwa washirika wa Ukraine, Marekani na Ulaya.

Ukraine ilianza kujibu mashambulizi ya Russia mwezi uliopita, ikikusudia kuyachukua tena maeneo yanayokaliwa na Russia tangu Russia ilipofanya uvamizi Febrauri 2022.

Maafisa wa Ukraine wameomba risasi na silaha zaida za kisasa, ikiwemo mifumo ya ulinzi wa anga na ndege za kivita, ili kulingana na uwezo wa jeshi la Russia.

Alisisitiza kuelezea suala lake kwa Ukraine kupatiwa ndege za kivita aina ya F-16, akisema kuwa na ndege siyo kwa ajili ya kupata fursa ya angani, lakini ni “kuwa na uwezo sawa” na jeshi la Russia.

Denmark ilisema wiki iliyopita kuwa mafunzo kwa marubani wa Ukraine kutumia ndege za F-16 yameanza.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG